Welcome PDF Print E-mail

Waadventista wasabato hupokea biblia kama kanuni ya pekee na kushika baadhi ya kanuni ya misingi ya imani kuwa ndiyo mafundisho ya maandko matakatifu. Imani hizi kama zilivyoorodheshwa hapa hufanya welekevu wa kanisa na udhihirisho wa mafundisho ya Maandiko. Masahihisho ya kauli hizi yanaweza kutegemewa katika kikao cha Halmashauri kuu wakati kanisa likiongozwa na Roho Mtakatifu kwenye ufahamu ulio kamilika zaidi wa ukweli wa biblia au linapopata lugha iliyo bora zaidi ya kuelezea mafundisho ya neno takatifu la Mungu.

.                                 

Normal 0 false false false EN-US X-NONE X-NONE MicrosoftInternetExplorer4

MAANDIKO MATAKATIFU

Maandiko matakatifu yaani agano la kale na agano jipya ndiyo neno la Mungu lililoandikwa likatolewa kwa walionena na kuandika kama walivyoongozwa na Roho wa Mungu.Ndani ya neno hili Mungu amemkabidhi mwanadamu ma arifa yaliyo lazima kwa ajili ya wokovu.Maandiko Matakatifu ni ufunuo usioweza kukosa wa mapenzi yake.Ndiyo upeo watabia,kipimo cha uzoefu,ufunuo dhabiti wenye mamlaka wa mafundisho ya imani na kumbukumbu aminifu ya matendo ya Mungu katika historia(2pet.1:20,21;2tim3:16,17: zb199;105; mith30:5,6;Isa8:20;1wathe2:13; waeb4:12)

UTATU MTAKATIFU

Kuna Mungu mmoja: Baba Mwana na Roho Matakatifu Umoja wa tatu za milele.Mungu hapatikani na mauti mwenye nguvu zote,ajuaye yote,zaidi ya yote na aliyeko daima.Yeye hana mwisho na nizaidi ya ufahamu wa kibinadamu,hata hivyoanafahamika kupitia kujifunua kwake binafsi Milele yote yu astahili kuabudiwa,kusujudiwa, kutumikiwa na viumbe wote.(kumb6:4;math28:19;2waef 4:4-6; 1tim 1:17 Ufu14:7)